Vita vya Ukraine: Je, uvamizi wa Ukraine umeanza? Wanajeshi na wataalamu wanasema nini juu yake

July 2024 · 6 minute read

7 Juni 2023

Idadi ya wanajeshi wa Ukraine iliongezeka katika mikoa ya Donetsk na Zaporozhye. Wizara ya Ulinzi ya Urusi Jumapili jioni ilisema kwamba Ukraine ilijaribu kushambulia kuelekea Donetsk Kusini, jimbo ambalo linadaiwa kukaliwa na vikosi vya Urusi.

Lakini , "waandishi wa habari wa kijeshi" wa Urusi na watu wanaounga mkono jeshi hilo wasiodhibitiwa na Wizara ya Ulinzi wanaripoti mapigano makali na kusonga mbele kwa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine katika maeneo tofauti katika mikoa ya Donetsk na Zaporozhye.

Mafanikio ya ndani ya vikosi vya Ukraine pia yanathibitishwa na vyanzo huru.

Ripoti ya mwakilishi wa Wizara ya Ulinzi wa Urusi, Jenerali Igor Konashenkov, inazungumzia kuhusu mwanzo wa mashambulio ya Ukraine katika maeneo matano ambayo wakati mmoja yalikuwa uwanja wa mapigano.

Inasemekanamapigano hayo yalianza Jumapili asubuhi, yakihusisha "vikosi sita vya adui vilivyo na mitambo na vikosi viwili vya vifaru" kwa jumla. "Adui hakufikia malengo yake. Hakukuwa na mafanikio," Konashenkov alisema.

Kwa upande wake Urusi inadai kwamba katika juhudi za kuwarudisha nyuma, wanajeshi wa Ukraine waliuliwa 250.

Jeshi la Ukraine bado halijathibitisha kuanza kwa mashambulio hayo, na limezitaja ripoti za idara ya Urusi "operesheni ya habari - kisaikolojia." "Ili kuwakatisha tamaa Waukraine na kupotosha jamii (pamoja na idadi yao ya watu),

Limesema Warusi wataeneza propaganda za uongo kuhusu athari mbaya kwa majeshi ya Ukraine.

‘’ Kwa hili, video za zamani na picha zimetayarishwa zinazoonyesha vifaa vilivyoharibiwa vya wafu na wafungwa, pamoja na vifaa vingine bandia," taarifa ya Idara ya Mawasiliano ya Kimkakati ya Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine inasema.

Hushambulia kwa njia tofauti

Wakati huo huo, ripoti za "waandishi wa kijeshi" wa Urusi kutoka uwanja wa mapigano zinaonekana kutisha kwa upande wa Urusi.

"Vita vikali vinaendelea hivi sasa katika kijiji cha Novodonetskoye, kilicho kando ya mstari wa mapambano ya kivita uliopo karibu kabisa katikati kati ya Ugledar na Velikaya Novoselovka," kiliandika kituo cha televisheni cha kijeshi cha Urusi -WarGonzo.

“Tangu asubuhi na mapema, mapigano makali yamekuwa yakiendelea baina ya pande mbili,” asema mwanapropaganda mwingine Mrusi Alexander Kots. “Baada ya kushindwa jana, adui aliingiza wanajeshi wengi kutoka magharibi na kuyapeleka hadi upande wa Ugledar.

Labda kwa lengo la kuzunguka kutoka kusini, Hata hivyo, Kiev inaweza kujaribu kwenda chini, kuelekea Nikolsky na Mangushev, na kuelekea Volnovakha, ili kugawanya DPR katika sehemu mbili.

"Adui pia anaendesha operesheni kijeshii katika eneo la Artemovsk. Mizinga imewekwa kaskazini mwa mji wa Soledar.

Mapigano pia yanaendelea kusini-magharibi mwa Bakhmut," ameandika Kots.

“Vikosi vinatembea kimya kimya”

Kusonga mbele kwa vikosi vya Ukraine karibu na Vuhledar pia kunathibitishwa na kamanda wa kikosi cha Vostok cha DPR anayeitwa Alexander Khodakovsky.

"Kwa upande wa kushoto wa Ugledar, adui, ambaye alikuwa na vichache, akitumia hadi magari kumi ya kivita, aliendeleza mashambulizi kuelekea upande wa Zolotaya Niva – Novodonetskoye na hadi sasa amepata mafanikio "., alisema, na kuongeza kuwa: "Upelelezi wa anga ulirekodi harakati za hadi magari thelathini ya kivita katika eneo hilo, lakini kwa sababu ya uwezo mdogo, hawakuweza kuanzisha hatua ya "kupanda."

Na mkuu wa Wagner PMC, Yevgeny Prigozhin, alitangaza kurudishwa nyuma kwa askari wa Urusi kaskazini mwa Bakhmut.

Taarifa ya hivi punde kutoka kwa Taasisi ya Utafiti wa Vita ya Marekani (ISW) inasema kuwa mnamo Juni 4, vikosi vya Ukraine vilifanya mashambulizi ya ardhini na kupata ufanisi mdogo wa kimbinu katika sehemu ya magharibi ya mkoa wa Donetsk na sehemu ya mashariki ya mkoa wa Zaporozhye.

Picha za eneo la ardhi zilizotolewa mnamo Juni 4 zinaonyesha vikosi vya Ukraine vinavyotumia mitambo vikisonga kaskazini mashariki mwa Rivnopol, wataalam wa kijeshi walisema.

Walitathmini kwa umakini ripoti za baadhi ya wanablogu wa Urusi wanaounga mkono jeshi kwamba wanajeshi wa Ukraine walikuwa wameweza kupenya safu ya kwanza ya ulinzi wa Urusi na kusonga mbele kwa kilomita 3 katika eneo hilo.

Vyanzo vya Idhaa ya BBC ya Kiukraine katika miundo rasmi ya vinasema kuwa hakuna mtu atakayetangaza kuanza kwa mashambulizi hayo. Vikosi vya Ukraine vinasema kuwa, vitajaribu kuusukuma mbali ulinzi wa Urusi katika sekta mbalimbali na kwenda kwenye mashambulizi ambapo ulinzi huu ni dhaifu zaidi.

Je, operesheni hii itageuka kuwa mashambulizi makubwa?

Oleg Chernysh , mwandishi wa BBC News Ukraine:

"Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi haijaelezewa nchini Ukraine au inatolewa maoni kwa maana kwamba ilikuwa operesheni ya habari na kisaikolojia. Kulikuwa na ujumbe kutoka kwa idara ya mawasiliano ya kimkakati ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ambayo Urusi ilikuwa imetayarisha.

Wakati huo huo, lea asubuhi na jana jioni, baadhi ya wanajeshi wa Ukraine, wanajeshi wa kujitolea na watu waliopo karibu na maeneo ya mapigano, walianza kueneza ujumbe usio na utata kwenye mitandao ya kijami uliosema: "Imeanza!", "Mungu awabariki!", "Twende!" Nakadhalika.

Kwa kawaida, tunaweza kudhani kwamba tunazungumza juu ya mashambulio ya Ukraine yaliypangwa dhidi ya Urusi. Kwa kuongezea, katika muktadha huu, ujumbe kutoka kwa wale wanaoitwa "waandishi wa kijeshi" wa Urusi ni muhimu, na vile vile Alexander Khodakovsky, mtu anayehusika katika mitandao ya kijamii ya DPR aliyejitangaza, kamanda wa zamani wa uwanja wa mapigano.

Ujumbe wao sio mzuri kama ule wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Wanathibitisha habari kwamba katika eneo karibu na Velyka Novoselka (mji mdogo kwenye mpaka wa mkoa wa Zaporizhia na Donetsk, sio mbali na Vuhledar), wanajeshi wa Kiukreni walianza kusonga mbele kwa mapigano, wakiwa na takriban brigedi mbili au vita nane, na katika eneo hili inadaiwa waliweza kusonga mbele kilomita kadhaa.

Kulingana na Taasisi ya Marekani ya Utafiti wa Vita, awali jeshi la Ukraine lilisonga na kufika hadi kilomita tatu upande wa Urusi , ambalo, katika hali ya vita hivi, kwa kuzingatia eneo la kuchimbwa, lililojaa silaha, ni umbali mkubwa.

Hilo linaonyesha kuwa , kuna harakati kwenye eneo hilo la mapigano , lakini huenda, isitoshe kwa vikosi vya Ukraine kukiita kinachotokea kuwa ni shambulio kubwa. Je, operesheni hii itageuka kuwa mashambulizi makubwa? Je, itakua zaidi? Wacha tuone kitakachofuata."

"Kuna kitu tayari kimeanza"

Na Profesa Michael Clarke, mchambuzi wa kijeshi, mkuu wa zamani wa Taasisi ya Utafiti wa Ulinzi wa Royal United (RUSI):

"Kwa maoni yangu, mashambulizi ya Ukraine yalianza wiki chache zilizopita - na mashambulizi ya pande zote kimya kimya kwa kutumia droni, na mashambulizi katika mwelekeo tofauti, karibu na Soledar, karibu na Vuhledar, karibu na Bakhmut, na katika eneo la Novodarovka huko Zaporozhye, kutokana na matukio ya yaliyoshuhudiwa kwenye mpaka wa pande mbili.

Pia kulikuwa na matukio ya kivita katika eneo la Shebekino katika mkoa wa Belgorod, ingawa hhayahusiano moja kwa moja na vitendo vya Kiev, lakini pia kumekuwa na hali ya uhasama unaoongezeka.

Kitu tayari kimeanza, hebu tuone jinsi kitakavyokua. Nadhani mnamo Juni 4, Waukraine walianzisha vita vya ardhini.

Kuna njia kadhaa za kuendelea mashambulio haya. Kwanza, inawezekana kwamba baada ya mapigano ya maeneo mbali mbali, athari nzima ya silaha zito za vikosi vya Ukraine zitaangyukia katika mwelekeo mmoja . Kingine kinachoweza kufanyika ni msururu wa mashambulizi. Ni kama wanatoka katika milango tofauti, na kuingia katika mlango unaofunguka kwa urahisi zaidi, watakimbilia ndani wote kwa wingi. Na uwezekano wa tatu ni msururu wa mashambulio madogo madogo, ambayo baadae yatageuka na kuwa kitu fulani zaidi. Hatutajua ni vipi mambo yatakavyoendelea, labda hadi wiki ijayo au hata wiki itakayofuata baadaye."

ncG1vNJzZmivp6x7o67CZ5qopV%2BoxKK0yKWgaJmiqbakuMSsZpywlWrFrrnVqamppw%3D%3D